UKURASA WA KITABU CHANGU

Maisha yangu ni mfano wa kitabu kilicho na kurasa nyingi zisiso hesabika,zipo kurasa zinazo vutia-ambazo zingekufanya udondoshe mate baada tu ya kuzisoma,pia zilivo nyooka unaeza sema ni msitari ,aidha zipo ambazo zimekunjika na kuchafuka ila sikuonelea nizichane bali nilizitumia kama funzo mana kisicho kuua basi kitakukomaza. Yote kwa yote,ningependa kuwasilimulia mojawapo ya kurasa zangu ambazo zilichochea moto na kupelekea mimi kujitosa katika tasnia ya utangazaji Huenda mtu yeyote angenijuza miaka kumi iliyopita,kwamba ninge tumbukia Kwenye huba na uandishi au utangazaji kwa ujumla,nafkiri ningebisha a u kudhani ni ndoto ambayo huenda ingebaki kuwa stori tu..Il a kwa uwezo wa Manani,safari hii ilipamba moto baada ya kujiunga na Chuo Cha kiufundi Cha Mombasa ( TUM ),chuo ambacho nilitamani sana kujiendeleza kimasomo nilipokuwa shule ya upili,si kwa sababu ni miongoni mwa vyuo 20 bora hapa inchini,pia nimeshuhudia watu mashuhuri na wenye wadhfa waki...