ALMASI YA KESHO
Kama safari ya kesho hupangwa Leo,kwanini kijana ambaye ni "kiongozi wa kesho"ashindwe kuandaliwa au kupewa uongozi katika muda huu.Licha ya haya yote, kijana ameendelea kudidimizwa na kunyimwa hata chembe ya fursa ambayo angeweza kuonyesha uwezo wake.Wasicho kijua ni kwamba, vijana wakifua dafu na kukwea kimaisha, hata uchumi wetu utashamiri na kuitupa hali ngumu ya maisha katika kaburi la sahau.
Picha kwa hisani ya iStock.com
Ndiposa,ningependa kuwajuza jinsi vijana wanaweza kuleta uamsho katika uchumi wetu.Ila kabla sijawaeleza,ni vyema tukajiuliza je,hali au uwezo wa vijana wetu unaruhusu?Hapana.Hii ni kwa sababu asilimia kubwa wanaishi maisha ya kutikisa kiberiti ili waone kama ndani Kuna njiti,wengine wakivikumbatia vibarua ambavyo labda huwapa milo miwili kwa siku,kwa wale waliokosa unafuu basi hutaa taa baada ya kukosa kabisa vibarua.
Tumezungukwa na vijana wengi ambao wamekata tamaa maishani,ndoto zao wakizitupilia mbali na kukosa matumaini mithili ya kuuwasha mshumaa palipo na upepo mkali wa kimbunga,bila shaka hautawaka.Kwa hali hii uchumi utaenuliwa kweli?ila pakiwa na watu au mashirika yakiongezeka zaidi na kuzunguka kutwa kucha ili tu yawahamasishe,nafuu utapatikana.Nahisi nafsi yangu itanisuta nisipo yapongeza mashirika ambayo husimama kidete na kujiza titi ili kuwahamasisha vijana.Kongole!
Vilevile,haki ikiwa sawa kwa wote-vijana wote wapewe fursa bila ya kubaguliwa iwe ni mke au mume,kwa aliye mzima au mlemavu basi hakuna kijana ambae atashindwa kuonyesha uwezo wake, mambo kama haya yakizingatiwa na kutekelezwa kwa ufaafu basi maendeleo yatadhihirika peupe.
Najua changamoto na vizingiti vinavyozuia vijana kushiriki katika maendeleo ya inchi ni vingi mno, ila suluhisho ni vijana waangaliwe na wapewe mkono utakaofanya wasimame,kwa walio wazidi umri,wawape nasaha na kuambia jinsi ya hao walivyo vishinda vizingiti hivyo,ingawa naamini hakuna mzee atakaye sema alikua mwoga utotoni,ila waambiwapo ukweli wataweza kusaidika zaidi
Huenda umejiuliza,ni vipi vijana wanaweza kuenua au kuboresha uchumi wetu basi ni kama ifwatavyo-
(I)baada ya kijana kupewa fursa,wapo wenye uwezo angavu wa kibiashara ambao wanaweza kubuni mbinu na kuuza bidhaa zetu kimataifa na kuliletea taifa pesa za kigeni
(Ii)kijana ataweza kulipa ushuru na mwishowe inchi kulipa madeni yake
(III)wapo watakao lipa fadhila na kuzalisha ajira kwa vijana wengine
(IV)kwa kudhihirisha uwezo wao, itachangia pakubwa uebukaji wa viwanda vitakavyo letea ichi njenje sufufu.
Hizi ni baadhi ya sababu ambazo zimetuonyesha tuna Kila sababu ya kuenua vijana wetu,tuhakikishe watang'aa kama almasi,mana wao ndio almasi yetu ya kesho.
"Sio Kila ambaye hajafanikiwa ni mvivu,maisha Yana Siri kubwa"
Imeandikwa na kuchapishwa na:
Sheban juma
Banniboy the presenter
Nakala nzuri
ReplyDeleteKubwa na Nusu
ReplyDeleteClean
ReplyDeleteKazi Safii
ReplyDeleteNakala Safii
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteVijana ndio funguo kuu ya uchumi
Kazi safi kaka
Allah akulinde na kila aina za Shari, na azidi kukupa ufahamu zaidi.. Allahumma Amiin 🤲
ReplyDeletekazi nzuri
ReplyDeleteKongolee kwa ufanisi huu mkaka
ReplyDeletewell done
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNimejiridhisha vilivyo niliposoma hii nkalala mwanzo mwisho, binafsi nasema kipaji na kipawa hiki kina stahili kukuzwa zaidi na kuweka sehemu husika ilayo stahili. Kijana huyu anastahili kuboreshwa zaidi ili awe muokozi wa vijana wenziwe mana ana ufahamu na weledi wa kupambanua shida za vijana wenziwe zilipo. Aliyasema yote yapo na nikweli kabsa, kwaiyo ombi langu mimi Kwa niaba yake naomba apawe futsal nafasi afanye zaidi ya anavyofanya sasa.
ReplyDeleteKazi safiii
ReplyDeleteSure bro
ReplyDeleteGreat 👌
ReplyDeleteMaashaallah,nakala smart Sana mwana Allah akulinde na hasad
ReplyDeleteNakala nzuri mdogo wangu,inshallah tutafika tunapolenga
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi murua👍
ReplyDeleteKazı safi
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteNice job
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNakala safi kaka 👏
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteBravo
ReplyDeleteBravo
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi safi na mbashara
ReplyDelete🔥🔥🔥🔥
ReplyDeleteWell written
ReplyDeleteWell written
ReplyDeleteHakikaaa
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteAmazing
ReplyDeleteIko sawa
ReplyDelete