HALI SIO HALI!

Kila mja angekuwa na uwezo wa kujichagulia maisha ayatakayo,basi hakuna ambaye angejitwika maisha yaliyo na fazaa au shida.Kila adinasi angejiweka mahali ambapo angefarijika zaidi.Mahali pasipo njaa,mafuriko,ukame,uwele au ugonjwa na mengineyo mengi yatakayo ikonga nafsi yake,chambilecho wavyele kujiudhi haifai roho haina thamani.

Je,ushawai jiuliza dhiki hizi huletwa na nini?Ngoja basi nikujuze,najua wapo ambao huenda wataviacha vinywa wazi,baada ya kujua kwamba, baadhi ya shida zinazotukaba hukaribishwa na hali ya hewa(ni athari hasi za hali ya hewa).

Ila "hali ya hewa" au halihewa imekua ikitafsiriwa kwa maana tofauti tofauti,wapo wanapolisikia basi fikra zao huchora mvua,jua au hata baridi shadidi,ingawa kitaaluma au kisayansi ni-namna ya kutaja yale yanayotokea katika sehemu ya chini ya angahewa, juu ya uso wa dunia katika eneo fulani na wakati fulani.(tafsiri hii ni kwa hisani ya Wikipedia).

Hali ya hewa ikiwa nzuri,basi mambo hunyooka mithili ya mstari.Ila ikizidi,yajayo huwa ni maafa,waama tamu ikipitiliza basi huwa sumu.Kwa mfano mvua ikinyesha kiasi,hata mimea hunawiri na mifugo kukata kiu chao,ila inapozidi kinachofwata huwa ni mafuriko ambayo husomba mali au hata kuharibu mimea.picha hii ni kwahisani ya iStock.com

Bila ya kupoteza hata akisami ya sekunde,ningependa niangazie baadhi ya athari za halihewa kwa uzaidi,athari kama- uhaba wa chakula-hii ni endapo halihewa imeathiri shughuli kama kilimo,chakula kinaeza patikana kwa uchache au kisipatikane kabisa.
Umasikini au uchochole-kama uchumi utadorora,kinachofwata huwa ni ufuska au umasikini.Uchumi utadorora vipi?Ikiwa mazao ni machache au hamna,na yasipo kuwepo,shughuli za biashara zitafanyika kweli?Na zisipo fanyika,wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo watapatapi fulusi?
Kuhama-kuna mida changamoto zinapo zidi unga,kunawa mikono huwa suluhisho mbadala,vivyo hivyo kwa anayeishi mahali ambapo kutwa kucha hakuishi mafuriko au ukame,wengine huamua kwenda sehemu nyengine hata kama kutawagharimu au ni mbali zaidi,kwani heri nusu Shari kuliko Shari kamili.
Matatizo ya kiafya-chakula kikiwa hafifu, basi muathiriwa anaeza patwa na lishe duni,aidha wapo ambao baridi Kali huwadhuru na mwishowe kupata homa.
picha hii ni kwahisani ya iStock.com

Unaposema kuwa wewe huna viatu, basi jua Kuna mwenzako ni kilema.Kwani anayetolea chozi hali ya mvua au jua,yupo mwenzako anayenyong'onyezwa na baridi Kali.Nakumbuka kama juzi tu,ilikua mwanzoni mwa huu mwaka,ambapo wavuvi katika maeneo ya pwani waliambulia hasara,hii ni baada ya kushahuriwa kutoenda baharini,kwa sababu ya upepo mkali ambao ungesababisha dhoruba katika bahari hindi-kulingana na TAIFA LEO,katika kaunti ya Lamu wavuvi takriban 9000 waliathiriwa na dhoruba iyo.Inasikitisha!

Najua ya kwamba,mabadiliko ya halihewa yamekua tatizo katika sehemu tofauti tofauti hapa inchini,kuchangia athari kama baa la njaa,japo tunaamini ya kwamba deni la tumbo halilipiki,tushikaneni pamoja na kuwapa pambaja.Si serikali tu,hata kwa yeyote mwenye uwezo.
Yote kwa Yote,tuwaaminishe walioathirika ya kwamba hawafai kunywa jasho mana maji yapo mbele!

Imeandikwa na kuchapishwa na
Sheban juma
Banniboy the presenter


Comments

  1. Hongera ,na Allah azidi kukupa ufahamu zaidi InshaAllah 🤲🤲🤲

    ReplyDelete
  2. Mashaallah! Allah azidi kujalia kipaji chako inshaallah amiin

    ReplyDelete
  3. Masha Allah,sky is the limit daddy

    ReplyDelete
  4. Masha Allah kila hatua dua kaka

    ReplyDelete
  5. Kazi safi sana kijana hongera

    ReplyDelete
  6. Kazi nzuri sana mungu hawazidishie inshaallah 🙏

    ReplyDelete
  7. Kweli kabisa ila mbadiliko ya tabia nchi kwa sasa ni janga linalo athiri dunia yote. Tujitahidi kuhakikusha tupo mahali pema.
    Kazi safi kaka

    ReplyDelete
  8. Inchi inahitaji wataalamu wenye vipaji na upeo wa kuchanganua maswalala tata kama haya, binafsi yangu natoa kongole nyingi Sana Kwa mchapishaji wa hili jaridi, Kwa kututoa wengi wetu masikio taka. Iwapo tahasisi husika zitazingatia haya yote yaliyo chapishwa hapa, basi sioni sababu kwanini huyu mchapishaji musimtafute ili awe msaidizi wenu wa mambo fulani mana yuwastahili kuwepo na nyinyi kimafanikio. Hongera sana kijana, mungo akupie kila tarajio lako Inn sha Allah....

    ReplyDelete
  9. Hongera kazi nzur bro

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI BOVU HALIFICHIKI

UKURASA WA KITABU CHANGU