masaibu yanayo wakumba vijana katika jamii
Ni changamoto sufufu zinazo wakumba vijana katika Karne hii,ila kabla hatuja zungumzia masaibu au changamoto hizo.Je,kijana ni nani?au anapaswa kuwa na miaka Kama mingapi? Maana au tafsiri zipo nyingi ila iliyo wazi na kujulikana na wengi ni-muda katika maisha ya adinasi/mtu kati ya utoto na utu uzima ususan miaka 15 hadi 29.
Katika muda huu vijana hupitia masaibu lukuki,wengine huamua kukata tamaa ila wengine uamua kujiza titi na kupambana nazo.Ila leo tutazungumzia machache.
Changamoto zenyewe ni kama zifwatazo
1.ukosefu wa ajira
2.dawa za kulevya
3.shinikizo la rika
4.wasiwasi wa muenekano wa kimaumbile
5.maswala ya kifamilia
6.uhalifu
UKOSEFU WA AJIRA
Swala hili limekua tatizi au tuseme kitendawili kisicho mteguzi miongoni mwa vijana wengi.Asilimia kubwa wamekua wakinyong'onyezwa na swala hili,wapo ambao walibahatika kusoma hadi chuo kikuu tena kwa kupata alama za kukonga roho za wengi,aidha wapo ambao hawakufua dafu masomoni hivyo basi kutokidhi matakwa ya muajiri,huenda.Fauka ya hayo katika Karne hii ya sasa inasemekana ili upate ajira basi unapaswa kujuana na baadhi ya wakurugenzi watakao chochea moto kwa mabwenyenye husika ili upate ajira, au kwa jina linalojulikana mitaani koneksheni.je kama huna koneksheni? Ingawa naamini kuwa mtazamo huu auzingatiwi na Kila muajiri wapo wanaoamini kuwa Anayestahiki apewe, na heshima ya mtu ni utu.
Yote tisa ,kumi ni vijana wanapaswa
kupambana na kuamini kuwa siku yao inakaribia,wajaribu mbinu tofauti tofauti (halali)za kujipatia riziki.Hata kama ni kupitia uchuuzi au ujasiria mali maana unapojituma neema uwa inakaribia.
DAWA ZA KULEVYA
Ni janga ambalo limeathiri wengi, hivyo basi kuadimisha ndoto zao mithili ya maziwa ya kuku.Vijana wengi huanza kama starehe na mwishowe kuwa waraibu,baada ya kuathirika na madawa haya wengine huzitelekeza familia zao,wengine huacha shule,wengine kudhohofika kiafya na maji yanapozidi unga huishia kuipiga teke dunia.Inasikitisha!
Ingawa kwa kizazi hiki usipotumia uraibu au ulevi wowote unaonekana mtu dhaifu, kumaanisha utumiaji umechukuliwa kama swala la kawaida.swali ni je, sote tukibebwa na mawimbi ya mihadarati nani atamuajiri wengine?Au hata kumuongoza mwengine?
SHINIKIZO LA RIKA
Shinikizo..kwa kiasi kubwa huwa miongoni mwa vijana wenyewe.wapo wanaoshakiza wenzao dhidi ya uraibu,wengine jinsi ya kuishi -ususan maisha ya ghali au gharama ya juu ,wengine pia hushakizwa na kubadili jinsi wanavyovaa ,na mengine mengi. Kama wewe ni bendera hufata upepo basi utaishia kufwata nyayo ambazo si sahihi,hivyo basi Imani thabiti ndio itakayo kufanya ustawi,kwa hiyo hata hali iwe mbaya mno kijana anapaswa kuimarisha msimamo wake.
Shinikizo la rika limezua matatizo mengi kwa kweli-vijana kupotoka kimaadili,kutengana na aila au familia zao na mengineyo.Ili kufika mbali hupaswi kufwata Kila unachoambiwa, haswa unapojua fika yatabatili juhudi zako kimaendeleo.
WASIWASI WA MUONEKANO WA KIMAUMBILE
Au kwa lugha nyengine kutojikubali kimaumbile.Vijana wanapo balehe Kuna mabadiliko ya kimwili yanayofanyika ,wapo wanaoridhishwa na mabadiliko hayo,wapo hudhirika mwanzoni alafu baadae kutoridhika, baada ya kupata maoni au shinikizo kutoka kwa wengine,na wapo ambao hawaridhishwi kabisa.
Tumesikia na kushuhudia kesi nyingi ambazo watu hupoteza maisha,au hata kujipa ulema wa maisha baada ya kutaka kubadilisha maumbile ila habari hizi kwa wengine zilikua kama kelele za chura aziwazuii kuendelea kutafuta vidonge na sindano za kubadili umbo lao,japo kuvipata ni gharama ila kwao si tatizo kwani hawajui kua hakuna mja kamili, na hujafa hujaumbika.
MASWALA YA KIFAMILIA
Wapo vijana wanao amua kujitweka mzigo ambao hukosa mtu atakaye utua, hii ni kupitia dhiki za kifamilia kama ufuska au uchochole unaombidi kufanya kazi kwa umri mdogo ili tu akamilishe mahitaji au matilaba ya nyumbani,aidha wapo ambao walikosa malezi ya wazazi wote wawili,hii ni labda kupitia utengano dhidi ya wazazi au kwa bahati mbaya kutangulia mbele za haki,Hali hii huweza kuchangia ukuaji duni wa muathiriwa na endapo atakosa usaidizi basi ,kijana huyo anaeza kosa muelekeo wa kimaisha.
UHALIFU
Ingawa wapo vijana wanaosema ni sababu ya ukosefu wa ajira ndio unaochangia wao kuwa wahalifu ila je, ilo ndio suluhisho?vijana wanapaswa kuamka na kufanya kazi yoyote halali(wasichague kazi)kwani kama kulima huwezi aimanishi usijaribu hata kurina,jitume.Sababu zengine zinazochangia ni kama matumizi ya dawa za kulevya,shinikizo la rika na mengineyo mengi
Vijana ndio tegemeo na viongozi wa kesho usikubali kitumika vibaya,jilinde,jitunze wewe ni wa THAMANI
IMEANDIKWA NA KUCHAPISHWA NA SHEBAN JUMA
(BANNIBOY THE PRESENTER)
Kazi safi
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteGreat work bro... keep it up
ReplyDeleteNzuri ruza aisee🔥🔥🔥
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKazi nzuri
Kazi safi
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteMashaallah bro ongera unastahili zawadi nono...mungu azidi kukufungulia
ReplyDeleteShukran kaka
DeleteMashaAllah simulizi nzuri sana❣️Allah akuzidishie ufahamu,tuweze pata simulizi nzuri zaidi na zaidi🤲🤲🤲
ReplyDeleteAmiin InshaAllah ♥️🤲
DeleteBig up brother💯unaweza💪🏽
ReplyDeleteShukran kaka
DeleteYouths are the one to built The Nation
ReplyDeleteExactly
DeleteJe uko tayari
ReplyDeleteMalezi pia huwa na changizo kubwa katika kuelekeza maisha ya mtoto. Malezi mazuri wakati mwingi huchangia ukuaji wa tabia njema kwenye jamii.
ReplyDeleteNakubaliana na ww
DeleteUmeeleza vizuri kabisa
ReplyDeleteNice work
ReplyDeleteKijana uko juu
ReplyDeleteSafiiii
ReplyDeleteVijana Wengi Wamejitosa Kwenye Lindi La Anasa
ReplyDeleteMashallah Tabarakallah kazi nzuri mwanangu Allah akuongezee kipaji zaidi
ReplyDeleteAmiin InshaAllah
DeleteNakala nzuri.
ReplyDeleteMufti📝💯
ReplyDeleteKaz Safi kaka
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteSafii
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteUkweli kuntu....hivi ndivyo mambo yalivyo
ReplyDelete