TUMEPATA MWANGA BAADA YA KIZA KINENE
Unapoizungumzia Mombasa,vitu sufufu hujijenga katika fikra yako,vitu kama;fuo za bahari,kivuko Cha feri bila kusahau pembe kubwa za alumini zilizojengwa kama kumbukumbu ya binti mfalme Margaret baada ya kuizuru Mombasa.Ndio! nazungumzia yale mapembe makubwa mawili yanayo patikana katika barabara ya Moi avenue.
Ila fauka ya hayo,hivi unajua kipo kitu Cha thamani ambacho ni zaidi ya baraka kwa wakaazi wa Mombasa?hapa naizungumzia bandari,kwani uchumi wa Mombasa na bandari ni kama shilingi kwa ya pili au tuseme vimevaana mithili ya Pete na kidole.
Kwa miaka na mikaka,wakaazi wa Mombasa wamekua wakijivunia sana kwa uwepo wa bandari hiyo,hii ni kwa sababu ya ajira lukuki zinazo jitokeza na ukuzaji wa vipawa miongoni mwa vijana,kama unafikiri ni uongo basi muulize barobaro yeyote anaechezea timu ya Bandari f.c au ya mpira wa kikapu.Aha! tuna Kila sababu ya kuipenda bandari yetu.
Ingawa zipo bandari zenginezo,kama ile ilioko;Lamu,Malindi,kiunga,kilifi,Mtwapa,shimoni,Funzi na Tanga.inayopaa kama tiara au inayo ongoza ni hii yetu ya Mombasa,hii ni kutokana na umiliki wa vifaa Bora na vya kisasa.
Huenda sababu hizi ndizo zilizo ifanya ishikiliye nafasi ya tano(5) barani Afrika na nambari mia moja na kumi na saba(117)duniani kama bandari bora ya kontena(takwimu hizi ni baada ya uchunguzi uliyo fanywa na Marine insights).
kwa ubora uliopo katika bandari hii, lazima kazi zingekuwa nyingi ndiposa fursa kochokocho za ajira zingejitokeza,hivyo basi kuwa faidisha walioko karibu(wakaazi wa Mombasa) kwani aliyesema atanguliaye chanoni hukuzidi tonge alikuwa sahihi.
Nuru hii iliweza kutokomea ghafla baada ya baadhi ya operesheni zake kuhamishwa hadi naivasha(mwaka wa 2019).kiza Totoro kikatanda kwani wafanya kazi 2,987 walipoteza ajira uchumi nao ukaanza kudorora.kwa mujibu wa shule ya biashara katika chuo kikuu Cha Nairobi walieka bayana ya kwamba, Mombasa ilipoteza takriban bilioni 17.4,hapo ndipo nilipoamini ya kwamba aliyesema Ah! haifai maishani hakumaanisha.
Kwanini nisiseme ah! Kama mimi ndiye kichwa Cha familia na nimepoteza ajira,kwanini nisiseme ah! na mtoto wangu anahitaji karo au kwanini nisiseme ah! na mke wangu anadaiwa vikoba nilivyofaa Kuvilipa na muda huu Sina kazi wala bazi,hali kama hii ilikuwa kwa wale waliokuwa wakifanya kazi katika vituo vya mizigo ya kontena(CFs) pamoja na wasafirishaji(wa malori).
Siku zote chura hulia maji yakiwa machache,yakijaa halii.
Hali hii iliendelea kwa takriban miaka miwili,huku treni zilizo tumia reli ya kisasa(SGR)zikiendelea na uchukuzi na usafirishaji.Nani angejua kama ujenzi wa reli hizo zingekua sababu ya baadhi ya mahuluki kukosa ajira? Lakini si walisema uonapo moshi basi jua Kuna moto au aliyejamba,mngoje atakunya yote kwa yote majibu ya reli hizo yalidhihirika.
Wanasema ukiona huzuni unazidi jua neema ina karibia na baada ya dhiki faraja.Wakati wa kampeni rais William Ruto alisema ya kwamba akichaguliwa kama rais, basi angeregesha operesheni zote za bandari Mombasa.Ingawa wapo waliodhani ilikuwa ni siasa tu,ila baada ya kuchaguliwa alidhihirisha kweli yeye ni mtu wa kusema na kutenda maana shughuli zote zimerudi nyumbani.Hivyo basi,nitakua mchoyo wa fadhila nisipotoa shukrani zangu za dhati kwa bwana rais,ndiposa nasema ahsante! Asante kwa kuregesha tabasamu kwa waliopoteza ajira na kwa wana Mombasa kwa ujumla.
Tukutane bandarini
IMEANDIKWA NA KUCHAPISHWA:
SHEBAN JUMA
BANNIBOY THE PRESENTER
IG: banniboy the mcee
Kaka naona hii "Ah!" imetoa taswara kamili ya maisha ya wapwani.
ReplyDeleteKazi safi kaka
kazi nzuriππ
ReplyDeleteKazi nzuri kaka
ReplyDeleteNjema
ReplyDeleteNdo hivo ushaweka wazi mambo ya kaunti ya Mombasa
ReplyDeleteKazi nzuri kaka
ReplyDeleteKazi Safi kaka
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteThis is Mombasa and Mombasa is our Business
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKaz murua na yenye kuridhisha
ReplyDeleteKazi nzuri ndugu
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNzuri
ReplyDeleteShukran sana
DeleteKazi kuntu
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteπ―π―π―kazi nzuriπ
ReplyDeleteShukran π
DeleteWazii mtu wanguπ₯
ReplyDeleteGood work π
ReplyDeleteKazi nzur bro...mungu azidi kukuongoza ..inshaallah amiin
ReplyDeleteChapisho nimeinarika na ujumbe uko sahihi kabsa, hongera Sana Kwa kazi safi kijana, mungu akutangulie kwa kila jambo lako inn sha Allah...
ReplyDeleteAmiin InshaAllah
DeleteCould not have been said any better
ReplyDeletePia sisi twaomba Mombasa yetu I've na mafanikio bora zaid
ReplyDeleteUsijali yote yatatimia kwa uwezo wa jaliya
DeleteKuntu kakaπππ
ReplyDeleteMasha Allah keep going bro
ReplyDeleteShukran
DeleteNice one
ReplyDeleteGood job kaka
ReplyDeleteSadakta.
ReplyDeleteUmejikakamua kuandika hili chapisho kazΔ± safi
ReplyDeleteVema kabisa. Walakini, vikomeshi hujatumia vizuri. Maandishi usomeka kwa urahisi panapo kuwa na uzingatiaji au uangalifu katika utumiaji wa vikomeshi (punctuation marks). Lakini umenena vema
ReplyDeleteShukran vyote vitarekebishika
DeleteCongratulations
ReplyDeleteHongera sana Jombzz
ReplyDeleteShukran jomba
Deleteπ₯π₯π₯π₯π―
ReplyDeleteπ₯π₯π₯π
ReplyDeleteKudoz Sheban kazi nzuri sana...
ReplyDeleteThanks sana
DeleteWow vizur
ReplyDeleteShukran sana
DeleteWaah unajua bro kaz safi
ReplyDeleteShukran sana
Deletewow that great boy big up.
ReplyDeleteRAJAB MWASARIAH
ReplyDeleteSimulizi nzuri kaka zenye mafunzo kumbukumbu na naelekezo
Endelea itimu kitabu tufurahiye kukiona kwenye soko