UKURASA WA KITABU CHANGU

Maisha yangu ni mfano wa kitabu kilicho na kurasa nyingi zisiso hesabika,zipo kurasa zinazo vutia-ambazo zingekufanya udondoshe mate baada tu ya kuzisoma,pia zilivo nyooka unaeza sema ni msitari,aidha zipo ambazo zimekunjika na kuchafuka ila sikuonelea nizichane bali nilizitumia kama funzo mana kisicho kuua basi kitakukomaza.
Yote kwa yote,ningependa kuwasilimulia mojawapo ya kurasa zangu ambazo zilichochea moto na kupelekea mimi kujitosa katika tasnia ya utangazaji
Huenda mtu yeyote angenijuza miaka kumi iliyopita,kwamba ningetumbukia
Kwenye huba na uandishi au utangazaji kwa ujumla,nafkiri ningebisha au kudhani ni ndoto ambayo huenda ingebaki kuwa stori tu..Ila kwa uwezo wa Manani,safari hii ilipamba moto baada ya kujiunga na Chuo Cha kiufundi Cha Mombasa (TUM),chuo ambacho nilitamani sana kujiendeleza kimasomo nilipokuwa shule ya upili,si kwa sababu ni miongoni mwa vyuo 20 bora hapa inchini,pia nimeshuhudia watu mashuhuri na wenye wadhfa wakifuzu katika chuo hicho,basi kwanini na Mimi nisiwe miongoni mwao?

Kabla ya kujiunga chuoni,nilikua na matarajio mengi sana,kama kuwa na marafiki sufufu-wasio hesabika,kutangamana na wenzangu na kufanya jambo kubwa la kihistoria, bila kusahau,kujipatia kigoli iwapo angetokea atakaye hutekenya moyo wangu,moyo unapocheka kwanini nikatae?

Fauka ya haya yote,niliamua kuwekeza nguvu nyingi katika masomo,kwani nialiamini huelewa wangu ndio ungenisaidia kufanikisha ndoto zangu,mana tunapo Jenga fikra ya mazingira tuliyo yaacha nyumbani,hatuna budi bali kujipiga moyo konde na kujiaminisha kuwa yote yatakuwa sawa,ingawa wapo watakao kukatisha tamaa wakiamini kuwa ng'ombe wa masikini hazai! Anazaa tena na kujibidiisha ili ampe ndama wake malezi bora 
Aliyesema kuwa maisha ya wanachuo si rahisi,alikuwa sahihi,mana nilijionea na kuyapitia yaani ukistaajabu ya Musa utaona ya comrade kunywa chai na karoti.Mimi mwenyewe pesa ya ada ilikuwa ikinipiga chenga,nishawai kosa mitihani Karibia Kila muhula na kunilazimu kufanya mitihani maalum, hali hii ya ukosefu wa ada ilipelekea nitafute vibarua ambavyo vingenipa angalau fulusi itakayo nisaidia kwenye ada.

Kuchanganya masomo na vibarua ilikuwa kibarua chenyewe,Muda niliuona kuwa mchache mno,nafikiri ndio mana sikupata marafiki wengi kama nilivyo tarajia,lakini wale marafiki kidogo nilio kutanishwa nao nilijenga nao uhusiano ulioshiba.

Ingawa wapo marafiki watakao kunyima fursa kwa sababu yakuhofia unaweza fanya vyema zaidi kuliko hao,pambana na uongeze kamba yako,mana kama wasemavyo Kila mbuzi hula kwa urefu wakamba yake.
kwa hisani ya iStock.com

Kila siku nilipokuwa chuoni,nilikumbuka kipindi ambacho baba yangu alikuwa akifungua redio,na kuamini ipo siku angeisikia sauti yangu,mama yangu ambaye ni mpenzi wa hadithi na simulizi aliamini kwamba ipo siku angesoma simulizi zangu.......


"Ukishajua ni nini unataka maishani,kipi kina hitajika ili ukipate,basi kamilisha mahitaji Kisha ukifwateπŸ₯‡"

Imeandikwa na kuchapishwa na
BANNIBOY THE PRESENTER
SHEBAN JUMA 


Comments

  1. Kazi yenye ubunifu ...ni matarajio yangu kwamba utaja kusoma kipindi kwenye radio

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Masha'Allah kakangu, May Allah open doors of success for you..you're so talented πŸ‘Œ...

      Delete
    2. Masha'Allah kakangu, May Allah open doors of success for you in sha'Allah... you're so talented πŸ‘Œ

      Delete
  3. Hongera sana ❣️ Mungu akulinde na kila aina ya Shari InshaAllah 🀲🀲🀲....Penye nia na njia itapatikana kwa nguvu zake Manani πŸ™πŸ™πŸ™.

    ReplyDelete
  4. Umeeleza kwa kina ipasavyo. Sadakta!

    ReplyDelete
  5. Mashallah Mashallah..Kazi nzuri sana broo

    ReplyDelete
  6. Nzuri wallah πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  7. Kazi safi sana. Mungu akujaalie kila lenye heri

    ReplyDelete
  8. Swadakta kazi nzuri bro

    ReplyDelete
  9. Kazi safi
    Usivunjike moyo kwani ndoto zako zitatimia tu

    ReplyDelete
  10. Ikiwa hii tahriri mdio yako ya mwanzo banu
    Mwezi mumhu akukunjulie akili uweze chapishe nzuri zaidi yahii
    Hii umegomga ndipp

    ReplyDelete
  11. Mashallah simulizi nzuri sana, unapolisoma unatamani liwe bado laendelea, halimuishii msomaji hamu kabsa. Hongera sana kijana, Inn sha Allah mungu akupe kila tarajio lako uyakidhi malengo yake uweke tabasamu kwenye nyuso za wazazi wako ili matajario yao dhiki yako yakamilike....

    ReplyDelete
  12. Looo Shabani, simulizi nzuri na kutia moyo. Manisha ni Barbara ndefu yenye mabonde, milima ngulai, mito na miteremko.Tunapoienda tujitahidi na kuvumilia tukitarajia kufika kileleni.
    Shaban you are a good writer may God bless you.

    ReplyDelete
  13. Swadakta ndugu Juma.nakumbuka Enzi hizo tukishindana kiswahili tukiwa katika chuo cha sekondari. Ilikuwa ni muhali Sana kukushinda ila namshukuru Mola kwa kuzidi kukuboresha na inshallah uzidi kunawiri.

    ReplyDelete
  14. Swadakta ndugu Juma.nakumbuka Enzi hizo tukishindana kiswahili tukiwa katika chuo cha sekondari. Ilikuwa ni muhali Sana kukushinda ila namshukuru Mola kwa kuzidi kukuboresha na inshallah uzidi kunawiri.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI BOVU HALIFICHIKI